November 20, 2020 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Gilles Muroto amezungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake kwa lengo la kuwashukuru na kuwapongeza Wananchi wa Mkoa huo kwa kuyasusia maandamano yasiyo na ukomo yaliyotangazwa kufanyika na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani wakidai kwamba uchaguzi mkuu uliofanyika October 28, 2020 haukuwa huru na haki.
“Niwashukuru wananchi wa Dodoma baada ya mchakato wa uchaguzi mkuu kufanyika, mtakumbuka kulikuwa na tishio la maandamano yasio na ukomo yaliyotangazwa na baadhi ya vyama vya upinzania na yote yalilenga nchi kutokutawalika lakini wananchi kwa ukomavu wao walisusia na hawakuona ni kitu cha maana kufanya hivyo, kipekee niwashukuru sana Wananchi kwa ukomavu wao” Kamanda Muroto
“Tanzania ni nchi ya watu ambao ni wakomavu na wanaelewa baya na zuri na yale mabaya waliyasusia baada ya kuyaona ni ya hovyo, wale waliokosa kura kwenye sanduku la kura baada ya kuona wanakokwenda ni giza wakaamua kutangaza maandamano na wananchi wakawapuuzia.”- Kamanda Gilles Muroto
“Kipekee nivipongeze pia vyombo vingine vya dola ambavyo tumekuwa tukishirikiana navyo katika kuhakikisha nchi imeendelea kuwa salama, wale waliolenga kwmaba nchi isitawalike sasa imetawalika na watu wote tuungane tukijua Tanzania ni yetu na hakuna aliye nje ya Tanzania kwahiyo tuendelee kushirikiana kwa pamoja kuilinda nchi yetu”-Kamanda Gilles Muroto