Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya, limeanza kutoa mafunzo ya matumizi sahihi ya silaha za moto kwa wamiliki binafsi, makampuni ya ulinzi na makampuni ya uwindaji ili kuhakikisha silaha hizo zinatumika ipasavyo na kwa kufuata sheria.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Ulrich Matei, amezindua zoezi hilo katika Wilaya ya Mbarali ambako zaidi ya washiriki 130 walihudhuria.
Ameainisha baadhi ya vipengele ambavyo wamiliki wa silaha wanafundishwa kuwa ni pamoja na ufunguaji na ufungaji wa silaha, namna sahihi ya kusafisha silaha, kanuni za umiliki wa silaha na ulengaji shabaha.