Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila ameliagiza Jeshi la Polisi kitengo cha Usalama Barabarani kuwakamata madereva wa magari na pikipiki za magurudumu matatu, maarufu kwa jina la Bajaji ambao hawatakuwa wameweka vitakasa mikono kwenye vyombo vyao vya usafiri.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amesema watu wanaowekwa karantini mkoani Mbeya sio wagonjwa wa corona bali ni wageni ambao wameingia nchini wakitokea nchi zenye mlipuko wa ugonjwa wa corona na wanatengwa ili kufanyiwa uchunguzi kwa muda wa siku 14 kwa lengo la kujiridhisha kuwa hawana maambukizi ya virusi hivyo.
KWA MARA YA KWANZA BARABARA ZA NJIA NNE ZAANZA KUJEGWA KIGOMA “TUMEZOEA KUZIONA KWINGINE”