Kamati ya Kudumu ya Bunge na Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) imefurahishwa na utekelezaji wa Maagizo kwa Serikali ambayo wamekuwa wakitoa mara kadhaa kwa mgodi wa STAMIGOLD uliopo wilayani Biharamulo Mkoani Kagera ambapo Mgodi huo hapo mwanzo ulikuwa ukitumia Zaidi ya Bilioni 1 za Mafuta kwa mwezi hali ambayo ilikuwa ikipelekea Mgodi huo kushindwa kujiendesha.
Hayo yameelezwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC) Vuma Augustino wakati walipotembelea Mgodi huo ambapo wametoa Maagizo kuhakikisha wanakamilisha Madeni yote ambayo walikuwa wakidaiwa kutokana mgodi kushindwa kujiendesha.
“Tumeshuhudia baadhi ya mambo yanaenda vzr jambo la kwanza tumeshuhudia kwamba sasa mgodi umeanza kutumia umeme kama chanzo cha Nishati kwenye shughuli zake na sio Mafuta tena ikumbukwe kwamba mara mwisho kuja hapa Mgodi ulikiwa ukitumia zaidia ya Bilioni 1 kwa mwezi kwa ajili ya Gharama za Mafuta lakini kwa sasa baada ya Maelekezo wa kamati kwa serikali waliharakisha mchakato ule na wakaunganisha umeme sahivi Mgodi unatumia nishati ya umeme kama chanzo cha nishati, ” Makamu Mwenyekiti Augustino.
Aidha Bw.Augustino kupitia kamati ya Bunge ya Kudumu ya uwekezaji na Mitaji ya Umma wameielekeza Serikali kupitia Mgodi huo kukamilisha Madai yote yanayodaiwa Bilioni 47 ambapo kiasi cha shilingi Bilioni 21.52 tayari kimeshalipwa.
Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalumu (CHADEMA) BI. Aidan Kanani ambaye pia ni Mjumbe katika kamati hiyo amesema ili kufikia Malengo ya uwekezaji Serikali haina Budi kuwekeza katika Utafiti huku akihoji Idadi ya watanzania walimopo katika kitengo cha Utafiti pamoja na Mkakati wa kuwapeleka wafanyakazi kupata elimu ya Mara kwa mara.
“Ili kufikia Malengo ya uzalishaji ya huu Mgodi lazima tuwekeze kwenye utafiti nategemea kabisa sisi hatupigi lamri kama kule kwetu sumbawanga sasa kama lazima tuwekeze kwenye kitengo cha utafiti nilitaka Kujua kwanza kitengo cha utafiti kina watanzania wangapi na Je mkakati wetu sisi wa kuwapeleka kupata elimu mara kwa mara ukoje, ” Mbunge Aidani Kanani.
Ally Ally ni Meneja wa Mgodi wa STAMIGOLD unaomilikiwa na Serikali amesema kwa Mwezi June Deni lilikuwa kiasi cha Shilingi Bilioni 47 mpaka kufikia Disemba wameshalipa kiasi cha Shilingi Bilioni 21.52 huku wakiwa na Mpango mkakati wa Kuendelea kupunguza Deni hilo.