Kulingana na ripoti ya awali iliyotolewa wikiendi hii, Kamati ya Kitaifa ya Usalama wa Uchukuzi (KNKT), rubani na rubani msaidizi walilala kwa wakati mmoja kwa dakika 28 wakati wa safari ya ndege kutoka Kendari Kusini-mashariki mwa jimbo la Sulawesi kuelekea mji mkuu Jakarta mnamo Januari 25 na kusababisha changamoto kutokana na ndege hiyo kutokuwa katika njia sahihi iliyotakiwa kuchukua.
Ndege hiyo ilikuwa na abiria 153 na wahudumu wanne kukiwa hakuna waliojeruhiwa wakati wa safari hiyo pia hakukuwa na uharibifu wowote kwa ndege, ripoti ya awali ya KNKT ilisema.
Safari ya ndege hiyo ilichukua masaa mawili na dakika 35 na ilifanikiwa kutua jijini Jakarta, kulingana na ripoti za shirika la habari la Antara. Kulingana na ripoti, rubani msaidizi alimjulisha rubani mwenzake mapema siku hiyo kwamba hakupata muda wa kutosha wa kupumzika.