Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa utekelezaji mzuri wa miradi ya Upangaji Matumizi ya Ardhi Katika vijiji.
Hayo yamebainishwa na Mwemyekiti wa Kamati hiyo Mhe, Timotheo Mzava wakati wa ziara ya Kamati kukagua utekelezaji miradi wa upangaji matumizi ya ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Ruangwa mkoa wa Lindi.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe, Geophrey Pinda ameiambia kamati hiyo kuwa Wizara yake itaendelea na utekelezaji mipango ya matumizi ya ardhi katika vijiji kulingana na upatikanaji wa fedha.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii imefanya ziara ya kukagua utekelezaji mradi wa kupanga matumizi ya ardhi katika kijiji cha Namkatila halmashauri ya wilaya ya Ruangwa . Aidha, Kamati pia ilikabidhi vyeti vya ardhi ya vijiji, ramani za mipaka iliyopimwa na kuhuishwa, mipango ya matumizi ya ardhi ya vijiji na Hati za Hatimiliki za kimila kwa wanachi.