Kamati ya kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma ikiendeshwa na mwenyekiti wa Kamati hiyo Deus Sangu imepokea maoni ya wadau kuhusu Muswada wa marekebisho ya sheria ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma.
Maoni hayo ya wadau yakipokelewa na kamati yatafanyiwa uchambuzi na baadae yatafikishwa bungeni na kuwa sehemu ya mapendekezo kwenye mabadiliko ya sheria baada ya muswada huo kusomwa kwa mara ya pili bungeno.
Novemba 10,2023 bungeni uliwasilishwa kwa mara ya kwanza Muswada wa marekebisho ya sheria ya uwekezaji na mitaji ya Umma lengo likiwa kufanya mageuzi ya kiuchumi katika uwekezaji.