Kamishna Jenerali wa Uhamiaji CGI Dkt. Anna Makakala amefanya ziara ya kushitukiza katika Uwanja wa ndege wa Kimatifa wa Mwl. Julius Nyerere (JNIA) uliopo Jijini DSM na kufanya ukaguzi wa pasipoti kwa wageni na raia waliowasili uwanjani hapo kwa ndege ya Shirika la Ethiopia.
Akiongea na waandishi wa habari uwanjani hapo CGI. Dkt. Makakala amesema amefika uwanjani hapo ikiwa ni moja ya ziara zake za kikazi ambapo hutembelea mipaka na vituo vya uhamiaji nchini kufanya ukaguzi wa mipaka na kukagua utendaji kazi wa Maafisa na Askari wa Uhamiaji katika maeneo yao ya kazi.
“Sisi Tanzania kama mnavyoiona tuna mipaka mingi sana, tumezungukwa na nchi takribani 8 ambazo mipaka yake ni mikubwa na mipana, lakini tupo katika mipaka yote, tuna vituo vya kutolea huduma za kiuhamiaji zaidi ya 80, hivyo tunawataka wageni wote na raia wa Tanzania kutumia utaratibu wa kuingia na kutoka nchini kwenye vituo vyetu vya kutolea huduma vilivyorasimishwa kwa mujibu w sheria na si vinginevyo” CGI Dkt. Makakala.
CGI Dkt. Makakala amesisitiza kwamba mtu yeyote atakae vunja sheria, ni lamiza sheria ichukue mkondo wake kwani haita angalia kwamba mgeni huyu au raia huyu ni kiongozi wa nyadhifa gani sheria ni msumeno inakata kote kote.
“Tupo kwenye kipindi cha uchaguzi Mkuu wa Rais Wabunge na Madiwani ni lazima tuhakikishe tunaumaliza uchaguzi wetu salama, lakini pia tumeongeza nguvu mipakani na kufanya doria na misako ya mara kwa mara ili kuilinda nchi yetu, nawaomba sana Watanzani tushirikiane katika kuilinda mipaka yetu kwani jukumu la ulinzi na usalama wa nchi yetu ni letu sote” CGI Dkt. Makakala