Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amempandisha cheo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Suzan Kaganda kuwa Kamishna wa Polisi.
Vilevile, Rais Samia amemteua Kamishna Kaganda kuwa Kamishna wa Utawala na Raslimali Watu wa Jeshi la Polisi.
Kamishna Kaganda anachukua nafasi ya Kamishna wa Polisi (CP) Benedict Wakulyamba ambaye atapangiwa kazi nyingine.