Raia wa Kenya aliyekutwa na hatia ya kesi ya mauaji nchini Saudi Arabia, Stephen Bertrand Munyakho, ameponea chupu chupu baada ya juhudi za nyuma ya pazia zilizofanyika dakika za mwisho na maafisa wakuu wa serikali kutoka wizara ya ya mambo ya nje ya Kenya pamoja na familia yake ili aachiwe huru na kuokoa maisha yake.
Stephen Betrand Munkho mwenye umri wa miaka 50 ambae ni Raia wa Kenya aliwekwa kizuizini miaka 13 iliyopita (2011) akiwa anatumikia hukumu ya kifo nchini Saudi Arabia mapema jana lakini maafisa wakuu wa serikali kutoka Kenya walihusika katika juhudi za kidiplomasia kuzuia jambo hilo kutokea.
Munkho alihamia nchini Saudi Arabia akiwa na aumri wa miaka 22 huku akifanya kazi za vibarua kupitia kampuni moja nchini humo kisha nchi hiyo katika falme za Kiarabu ndio yalikuwa makazi yake rasmi huku rekodi zikionyesha Munkho alijipatia hadi jina la Kiislamu na kuitwa “Abdulkareem.”
Munkho anayejulikana zaidi kama ‘Stevo’ alihusika katika ugomvi ambao uligeuka kuwa wa vurugu kubwa na aliyekuwa rafiki yake na mfanyakazi mwenzake Abdul Halim Mujahid Makrad Saleh. Katika ugomvi huo Saleh alichomwa kisu na kujeruhiwa, japo Saleh alikimbizwa hospitali hapo baadae alifariki dunia na huku Stevo akinusurika baada ya kupata majeraha ambayo hayakuwa hatarishi kwenye maisha yake.
Kesi ilianza na Stevo akapatikana na hatia ya kuua bila kukusudia na kuhukumiwa kifungo cha miaka mitano jela. Familia ya Saleh hata hivyo ilikata rufaa katika mahakama ya Shariah na kwa bahati mbaya ‘Stevo’ ambae ni baba wa watoto watatu alihukumiwa kifo.
Chini ya sheria za Kiislamu za “SHARIAH”, “malipo ya damu” hutumika kumlipa mwathirika au familia yake na malipo hayo yanaweza kutozwa kutokana na makosa mbalimbali ya uhalifu kama mauaji, majeraha ya mwili na uharibifu wa mali. Vinginevyo, “diya” au kinachojulikana kama “malipo ya damu”, yanaweza kulipwa kama fidia ya kifedha kwa mwathirika au mrithi wake katika kesi za mauaji, madhara ya mwili au uharibifu wa mali kimakosa. Katika kesi ya Stevo, ya kuua bila kukusudia familia ya Munkho alipewa chaguo la kulipa $2.6M kama fidia lakini baada ya makubaliano na mazungumzo ya pande zote mbili familia ya Saleh ilikubali adhabu ipunguzwe hadi $950M ambazo zilitafsiri kuwa na ndicho kiasi kinachopaswa kulipwa, kikamilifu, kabla ya Stevo kutolewa na kuachiliwa kwenda nyumbani.
Hivi karibuni mama wa kijana huyo ameongoza kampeni ndefu na ngumu ya kumuokoa mtoto wake kutoka kwenye adhabu hiyo na alipata ahueni pindi alipopewa muda wiki hii huku familia ikilazimika kuchangisha KSh150 milioni kama fidia, inaojulikana kama pesa za damu, ambazo ni kwaajili ya kulipa ili kuachiliwa huru au kijana huyo atanyongwa.
Kwa mujibu wa vyombo mbalimbali vya habari michango ya sasa imefikia angalau chini ya 5% ya $1m inayohitajika (£790,000), anasema Bi Kweyu, japo mazungumzo yameonekana kuwa ni marefu na magumu, wakitegemea serikali ya Kenya kutatua changamoto hii.
Mapema wiki hii, Katibu Mkuu wa Masuala ya Diaspora Kenya Korir Sing’oei alitangaza kwamba mamlaka ya Saudi Arabia imekubali rufaa ya Kenya ya kupinga kunyongwa kwa Munyango hadi tarehe ya baadae ili kutoa nafasi kwa mazungumzo zaidi.