Wadau na wanaharakati wa masuala ya haki za kimtandao hivi sasa wanawasiwasi kwamba Watanzania wanapoelekea kwenye Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwaka 2025 Serikali huenda ikachukua hatua za kudhibiti matumizi ya intaneti, hususani mitandao ya kijamii, ambayo inaweza kuhatarisha ukiukwaji wa haki za msingi za wananchi wake kama vile uhuru wa kujieleza.
Mitandao ya kijamii, hususani ile ya Facebook, WhatsApp, Twitter, na Instagram, imekuwa majukwaa mashuhuri kwa siku za hivi karibuni ambapo watu hutumia majukwaa hayo kuelezea hisia na maoni yao juu ya mambo mbali mbali yanayotokea katika nchi yao.
Katika kuliona hilo kupitia kampeni ya #KeepItOnTZ, ambayo imeanzishwa na Zaina Foundation imehakikisha kwamba Serikali haichukui hatua yoyote ya kuzima intaneti kwani inaweza kuwa na madhara makubwa katika ushiriki wa wananchi katika uchaguzi ujao.
Shirika la Zaina Foundation limejikita katika kuhamasisha wanawake juu ya matumizi salama ya mtandao likiamini kwamba matumizi ya intaneti ni haki ya msingi ya binadamu. Ni moja kati mashirika machache yanayoshauri Serikali kutozima mtandao wa intaneti, kwenye kampeni ya #KeepItOnTZ kufikisha ujumbe .
Mitandao ya kijamii, hususani Facebook, WhatsApp, Twitter, na Instagram, imekuwa majukwaa mashuhuri kwa siku za hivi karibuni ambapo watu hutumia majukwaa hayo kuelezea hisia na maoni yao juu ya mambo mbali mbali yanayotokea katika nchi yao hivyo ni muhimu mitandao kuwa inafikika wakati wowote.