October 24 2015 zimebaki saa chache mpaka sasa kuifikia October 25 siku ya Uchaguzi Mkuu wa Madiwani, Wabunge na Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, ni Uchaguzi ambao huwa unafanyika kila baada ya miaka kipindi mitano.
Kampeni zimefungwa rasmi leo, October 24 2015 katika Viwanja mbalimbali, nimefanikiwa kupata ripoti toka Viwanja viwili tofauti ambapo Mgombea Urais wa CHADEMA ambaye anawakilisha pia Umoja wa Vyama vya UKAWA, Edward Ngoyai Lowassa alikuwa kwenye Viwanja vya Jangwani Dar es Salaam, wakati huohuo Mgombea Urais kwa Tiketi ya CCM, Dk. John Pombe Joseph Magufuli alikuwa Mwanza, katika Uwanja wa CCM Kirumba.
HAPA NAANZA NA MZIGO WA JUKWAA LA UKAWA, JANGWANI DAR
Hizi hapa pichaz za UKAWA Jangwani Dar pamoja na nukuu ya baadhi ya maneno ya Edward Lowassa akifunga Kampeni.
“Tuna kila sababu ya kukubaliana na Mzee Kingunge kwamba CCM imeishiwa pumzi, haina uwezo kutufikisha kwenye kilele cha mafanikio… Tunapaswa kumuelewa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, alisema Chama kimoja kikikaa madarakani kwa muda mrefu kinajisahau.”>>> Edward Ngoyai Lowassa.
“Urais sio dhamana ya kutisha watu, ni wajibu wa kuongoza dira ya Taifa, anayeomba Urais anapaswa kuwa mtu aliyejiandaa… Watanzania tukubali mabadiliko.” >>> Edward Lowassa.
HAPA NAMALIZIA NA MZIGO WA CCM, UWANJA WA CCM KIRUMBA MWANZA.
Baada ya hapo nakusogezea na hizi kutoka Uwanja wa CCM Kirumba katikati ya Jiji la Mwanza… Dk. Magufuli na Mama Samia Suluhu Hassan wamesindikizwa na Viongozi pamoja na wanachama wa CCM kufunga Kampeni za Uchaguzi Mkuu leoleo.
Rais JK alipata nafasi ya kuongelea mambo machache pia wakati wa kufungwa kwa Kampeni hizo.
“Mtu kuhama CCM ni Chaguo lake, hatutohangaika kumuomba arudi… tuliopo tunatosha“– Rais Kikwete.
Haya ndio majibu ya Rais Jakaya Kikwete kuhusu ishu ya RICHMOND >>> “Kwenye RICHMOND tulikubaliana kwa pamoja kwamba kwa sababu Mabwawa yetu yamekauka, tukodishe Mitambo nje ya kuzalisha Umeme, mimi sikuhusika Kampuni gani ilete Mitambo… Tatizo kwenye RICHMOND Kanuni hazikuzingatiwa“
“Badala ya shughuli ile kufanywa na TANESCo, Waziri Mkuu aliunda Kamati yake ya Makatibu Wakuu ifanye hiyo kazi na kutoa taarifa kwake, ndio maana Tume ya Bunge ilimwambia yeye ndio Chanzo.. ndio maana siku moja nikamwambia Tundu Lissu kwamba mwenye RICHMOND yuko nae yeye.” >>> Rais Jakaya Kikwete.
“Waziri Msabaha aliwahi kuja akaniambia Wizara ya Fedha hawataki kutoa malipo ya kwanza kwenye hiyo Kampuni, mimi nikamwambia nawaunga mkono watu wa Wizara ya Fedha.. na nilimwambia Waziri Msabaha kuwa hiyo ni Kampuni hewa.” >>> Rais Jakaya Kikwete.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE.