Kampuni ya ulinzi ya Uingereza ya BAE Systems inasema ilianzisha shirika la ndani nchini Ukraine na kutia saini mikataba na serikali kusaidia kuongeza usambazaji wa silaha na vifaa vya Kyiv.
Hatua hiyo ya Alhamisi itaiwezesha BAE kufanya kazi moja kwa moja na maafisa wa Kyiv kuchunguza washirika watarajiwa wa mpango wa hatimaye kuzalisha bunduki nyepesi za mm 105, aina ya silaha za kivita, nchini Ukraine na kuelewa vyema mahitaji yake ya uwezo.
Kama mkandarasi mkuu wa ulinzi wa Uingereza, BAE imetengeneza vifaa vingi ambavyo Uingereza na serikali zingine zimetoa kwa Ukraini ili kuzuia uvamizi wa Urusi.
Uingereza ni muuzaji mkuu wa ulinzi wa Ukraine na mwezi Mei ikawa nchi ya kwanza kuanza kuipatia Kyiv makombora ya masafa marefu.
“Silaha bora ambazo kwa sasa zinawasaidia wapiganaji wetu kuilinda Ukraine zinapaswa kuzalishwa nchini Ukraine,” Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy aliandika kwenye X, zamani Twitter, kufuatia mkutano na Mtendaji Mkuu wa BAE Charles Woodburn.
“Uendelezaji wa utengenezaji wa silaha zetu wenyewe ni kipaumbele cha juu.”