Kampuni ya Adidas iliwapiga marufuku mashabiki wa kandanda kubadilisha jezi ya taifa ya Ujerumani kwa nambari 44 kutokana na kudhaniwa kuwa inafanana na nembo iliyotumiwa na vikosi vya SS vya Nazi wakati wa vita kuu ya pili ya dunia.
Schutzstaffel (SS), shirika la kijeshi la Utawala wa Tatu wa Adolf Hitler, lilipewa jukumu la kutekeleza mauaji ya kiviwanda ya Wayahudi kote Ulaya.
Wasiwasi juu ya jezi hizo hapo awali uliibuliwa na mwanahistoria Michael König, ambaye alisema muundo wa jezi hizo “unatia shaka sana”.
Seti ya ugenini ya Ujerumani pia ilizua utata kutokana pia na rangi yake.
Msemaji wa Adidas, Oliver Brüggen, alikanusha kwamba kufanana kwa jezi hiyo na nembo za Nazi kulifanywa kimakusudi. “Sisi kama kampuni tumejitolea kupinga chuki dhidi ya wageni, vurugu na chuki kwa kila namna,” alisema. “Tutazuia ubinafsishaji wa jezi.”