Kampuni ya Apple imeachana na matarajio yake ya kuzalisha gari la umeme, vyombo vya habari vya Marekani viliripoti Jumanne,
Kulingana na ripoti ya Bloomberg,kampuni ya kutengeneza iPhone iliwaweka karibu wafanyakazi 2,000 kwenye mpango wake wa siri wa kutengeneza magari hayo, lakini ilikabiliwa na sekta ya magari ya umeme (EV) yenye ushindani mkubwa.
Apple walikuwa wameripotiwa kuwekeza mabilioni ya dola katika mradi huo huku lengo la “Project Titan,”likiwa ni kuanzia mwaka wa 2014, lilikuwa kutengeneza gari linalojiendesha lenyewe kikamilifu.
Uamuzi wa kuzima ndoto za mradi huu wa magari ya umeme ulitangazwa Jumanne, na Bloomberg pamoja na The New York Times zikinukuu vyanzo ambavyo havikutajwa.