Nchini Japan kampuni ya Science Co. imebuni Mashine ya kuogea ya kisasa inayoitwa Mirai Ningen Sentakuki kwa kijapani ambayo inatumia Teknolojia ya akili bandia (AI) na mawimbi ya ultrasonic kuogesha mwili wa Binadamu pia Mashine hii yenye umbo la yai imeundwa ili kufanikisha si tu usafi wa mwili bali pia utulivu wa akili.
Wakati wa matumizi Mashine hii hujaza maji moto kwa kiwango kinachohitajika huku sensa maalum zikifuatilia mapigo ya moyo na hali ya mwili ya mtumiaji pia ina Teknolojia ya viputo vidogo ambavyo hufanya kazi ya kufanya masaji mwilini huku mfumo wa AI ukionyesha picha za pamoja na sauti za utulivu na harufu nzuri.
Kiongozi wa mradi huu Yasuaki Aoyama alisema wazo hili lilitokana na mfano wa Bafu linalotumia mionzi ya ultrasonic aliyoiona kwenye maonyesho ya Osaka mwaka 1970 hivyo Mashine hiyo ya kisasa sasa imeboreshwa zaidi na inatarajiwa kuonyeshwa rasmi kwenye maonyesho ya Osaka Kansai Expo mwaka 2025.
Wageni walio na nafasi wataweza kuijaribu mashine hiyo kwa mara ya kwanza huku Science Co. ikilenga kuleta mapinduzi makubwa katika Teknolojia ya usafi wa mwili na utulivu wa akili, hadi sasa maombi ya majaribio tayari yamepita matarajio yakionyesha hamasa kubwa kutoka kwa umma.