Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya Ireland (DPC) imeipiga faini ya takriban Tsh. Bilioni 273 Kampuni ya META baada ya kubainika ‘Passwords’ za Watumiaji Milioni 600 wa Facebook zilivujishwa kwa Wafanyakazi
Kwa mujibu wa taarifa, META haikutekeleza hatua madhubuti za kiusalama za Shirika ili kulinda Taarifa Binafsi za watumiaji dhidi ya Wadukuzi. Pia, ilishindwa kudhibiti hatari zinazoweza kuathiri taarifa zilizohifadhiwa katika ‘Seva’ zake
Tangu Mwaka 2018, META inakadiriwa kukumbwa na Kesi zaidi ya 8 za ukiukwaji wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, ambazo zimekuwa zikiigharimu Kampuni hiyo Mabilioni ya Fedha kupitia faini inazopigwa.