Application ya Nala iliyotengenezwa na Kijana Mtanzania Benjamin Fernandes imeweza kupata uwekezaji wa Bilioni 23.1 ($10 Million) kwa ajili ya kukuza huduma zake ambapo hii ni pamoja na kuzindua huduma zake kwenye nchi za Ulaya na Marekani na kutoa ajira kwa vijana wengi.
Kupitia uwekezaji huu, NALA imeweza kuweka rekodi nyingine katika sekta ya kampuni za teknolojia chipukizi (Startups) hapa Tanzania kutokana na uwekezaji huu mkubwa kuwahi kutokea.
Baadhi ya Wawekezaji wa NALA ni Watu maarufu kwenye sekta ya teknolojia na fedha duniani kama vile Jonas Templestein mwanzilishi wa Monzo, Vladimir Tenev CEO na mwanzilishi wa Robinhood, Peeyush Ranjan ambaye ni head of Google Payments.
Uwekezaji huu vilevile umeambata na hatua nyingine za mafanikio kwa NALA kama vile kupata leseni za kutoa huduma za kifedha Marekani na Umoja wa nchi za Ulaya pamoja na kuingia makubaliano ya kibiashara na moja ya benki kubwa duniani “Citi Bank Global”
Akizungumza na Ayo TV Benjamin amesema “Namshukuru sana Mungu kwa hatua hii kubwa ya mafanikio kwa NALA na Waafrika wote duniani. Nashukuru sana watumiaji wote wa NALA kwa support na kutuamini. Tutazidi kujikita katika kuwapa huduma bora za kutuma na kupokea fedha kutoka nje ya Afrika na Afrika. Huu ni mwanzo tu, mengi mazuri yanakuja”
MWIJAKU AFUNGUKA BAADA YA RAIS SAMIA KUPIGA SIMU NA KUTAJA JINA LAKE “MIMI RASMI NI CHAWA WA MAMA”