Bastola janja ya kwanza duniani “smart gun” ambayo inafanya kazi kwa kutumia mfumo wa alama za vidole na utambulisho wa sura ( finger print & facial recognition) imeingizwa sokoni nchini Marekani ambapo Watengenezaji wake wanasema mfumo huo wa kipekee utasaidia usalama zaidi na kuokoa maisha kwani silaha hiyo itakubali kufanya kazi baada ya kutambua sura ya Mmiliki pamoja na alama zake za vidole.
Silaha hii ya kisasa yenye urefu milimita 9 haitofanya kazi au kutumiwa na Mtu yeyote mwingine isipokuwa Mmiliki au Watumiaji walioruhusiwa na Mmiliki wa silaha hiyo ambapo Watengenezaji wake ambao ni Kampuni ya Biofire wanasema teknolojia hiyo ya usalama itaboresha na kuokoa maisha ya Watu nchini Marekani.
“Mtazamo wa Biofire ni mpya kabisa: tumetumia kanuni za uhandisi za usahihi wa hali ya juu ili kupunguza athari kubwa katika vifo vinavyoweza kuzuilika kwa kutumia silaha miongoni mwa watoto hakuna mtu aliyejaribu hilo hapo awali kwa sababu hiyo, Biofire sasa inatoa bunduki za watumiaji zilizobobea zaidi kiteknolojia. ” Kai Kloepfer, Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa Biofire.
“Hii ni enzi mpya katika usalama wa silaha inayoendeshwa na tamaa na matumaini, ikichochewa na wazo kwamba tunaweza kusaidia kuokoa maisha ya watu.”
”Kwa wamiliki wa bunduki wanaohusika na faragha, bunduki hutumia data ya kibayometriki ambayo haiachi kamwe bunduki, ambayo haina WiFi, Bluetooth au GPS ya ndani. Pia, vitambuzi vya Integrated IR kwenye mshiko huweka bunduki ikiwa na silaha wakati mtumiaji aliyeidhinishwa ameshikilia bunduki, hivyo basi huondoa hitaji la kuendelea kuthibitisha bayometriki zao”.
Bei yake $1,499 ambazo ni sawa na milioni tatu na laki tano pesa za Tanzania ina uwezo wa kufunguka tayari kwa matumizi ndani ya sekunde moja tu baada ya kutambua sura na alama za vidole za Mmiliki na ina uwezo wa kujifunga tena kwa haraka pindi matumizi yake yanapokamilika.