Kampuni ya usafirishaji abiria baharini ya Zanzibar Fast Ferries ambao pia ni wamiliki wa boti za Zanzibar I na Zanzibar II, imetangaza kusitisha safari zake kati ya Unguja na Dar es Salaam kuanzia Mei 27, 2020.
Hatua hiyo imechukuliwa baada ya maombi yao kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuhusu idadi ya abiria wanaopaswa kuchukuwa kutokujibiwa licha ya kuandika barua tangu Aprili 28, mwaka huu baada ya kuona wanaendesha kwa hasara.
Mmoja ya wakurugenzi wa kampuni hiyo, Salum Turki, amesema awali kulikuwa na muongozo wa Serikali kuhusu idadi ya abiria wanaopaswa kuchukuwa ambayo haikutakiwa kuzidi asilimia 50 ya idadi ya abiria wote.
Amesema kutokana na mazingira ya uendeshaji wa hasara, Aprili 28, 2020, walilazimika kuandika barua kwa Serikali kuomba nafuu lakini hawajajibiwa mpaka leo.
Jitahada zetu za kuupata upande wa pili zimeshindikana baada ya kumtafuta Katibu Mkuu Wizara inayohusika na uchukuzi bila mafanikio.
“RAIS MAGUFULI APEWE TUZO, NDUGAI AIANDAE WAKATI ANAFUNGA BUNGE” HAKI FURSA