Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa amesema kuwa mambo yote mazuri yaliyofanywa na mtangulizi wake, Dk.Harrison Mwakyembe katika sekta anazozisimamia atayaendeleza ili matarajio ya kuundwa kwa kwa Wizara hiyo yafikiwe.
Bashungwa wakati akipokea Ofisi kutoka kwa Waziri mstaafu Dk. Mwakyembe ambapo ameeleza kuwa ataendelea kushauriana na naye katika masuala mbalimbali ya wizara hiyo kutokana na uzoefu aliyonao, huku akisitiza kuwa mahusiano mazuri na watu katika maeneo mbalimbali ya kazi na jamii ni muhimu kwa sababu manufaa mengi.
“Tulishirikiana na wewe katika kuhamisha Taasisi ya Haki Miliki Tanzania (COSOTA) kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara kuja wizara hii,nimatumaini yangu tutaendelea kushirikiana katika sekta zote za wizara hii” Bashungwa
“Tayari nimeaviagiza Vyama vya Michezo kuwasilisha mpango mkakati wa namna ya kuendesha michezo nchini, pia suala la Makampuni ya Michezo ya Kubahatisha kuchangia katika ustawi wa Timu za Taifa,” Bashungwa.
Aidha, Bashungwa ameiagiza Bodi ya Filamu Tanzania kuona namna ya kuanzisha mfumo ambao utatumika kuuza kazi za filamu kwa mfumo wa kidigitali kama ilivyo ‘Netflix’ kwani itasaidia wasanii kusambaza kazi zao kwa urahisi na pia kuchangia katika pato la taifa ambapo alisisitiza kuwa “Msanii kiwanda chake ni kichwa chake,”.
JPM AMPA MAKAVU WAZIRI WA MICHEZO “TUKIFUNGWA UTAONDOKA NA NAIBU, SIMBA NA YANGA WAMETUCHELEWESHA”