Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo leo March 30, 2017 amezindua ujenzi wa mradi wa umeme wa maporomoko ya mto Rusumo ambao unatarajia kuwa na megawati 80 zitakazosaidia kuongeza nguvu ya nishati hiyo kwa nchi tatu, Tanzania, Rwanda na Burundi.
Mradi huo utagharimu U$D million 340 kutoka Benki ya Dunia, ambapo Benki ya Maendeleo ya Afrika itatoa U$D million 121, na baada ya mradi huo kukamilika kila nchi inatarajia kupata megawati 26.6.
Aidha, Prof. Muhongo amesema kuwa mradi huo unatarajia kukamilika February 2020 huku akitoa ufafanuzi wa fidia kwa wale watakaopisha mradi huo unaojengwa katika eneo la Rusumo lililopo Wilaya ya Ngara Mkoani Kagera mpakani mwa Tanzania na Rwanda.
VIDEO: Waziri Mwakyembe na Nay wa Mitego walivyokutana Dodoma
BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako MillardAyo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID na IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo