Kiongozi wa serikali ya kijeshi nchini Mali, Kanali Assimi Goita, amefanya majadiliano na rais wa Urusi, Vladimir Putin, kuhusu usalama na uchumi.
Kanali Goita amemshukuru Putin kwa msaada wa kibinadamu alioutoa pamoja na usaidizi katika kuhakikisha usalama na kupiga jeki mapambano dhidi ya makundi ya kijihadi nchini mwake.
Kupitia mazungumzo ya simu, viongozi hao wawili walizingatia haswa uhusiano wa kibiashara na uchumi, ikiwemo usafirishaji wa nafaka, mbolea na mafuta kutoka Urusi hadi Mali.
Kiongozi huyo kupitia ukurasa Wake wa twitter, amesema kuwa maungumzo yao pia yalijikia katika masuala muhimu ya kiusalama, kiuchumi na uhusiano wa kidiplomasia.
Mnamo mwezi machi na Agosti mwaka jana, Mali ilipokea msaada wa kijeshi kutoka Urusi msaada mwingine wa kijeshi ukiingia nchiini humo mwanzoni mwa mwaka huu.
Taifa la mali limekuwa likipambana na utovu wa usalama tangu kuzuka kwa makundi ya kijihadi katika eneo la Kaksazini mwa nchi hiyo 2012.
Tangu Agosti 2020 imetawaliwa na jeshi la kijeshi, ambalo lilivunja muungano wa muda mrefu na Ufaransa na washirika wengine wa Magharibi katika mapambano dhidi ya jihadism na kugeukia Urusi kwa usaidizi wa kisiasa na kijeshi.
Mali ilipokea usafirishaji wa vifaa vya kijeshi vya Urusi mnamo Machi na Agosti 2022, na tena mnamo Januari 2023.
Mnamo Machi, jeshi la Mali lilipokea ndege kadhaa kutoka Urusi.