Kanisa la City Christian Center(CCC) – Upanga, limewaka Viongozi wa taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi kuishi katika misingi ya maadili, kuanzia ngazi ya familia hadi wanapotekeleza majuku yao.
Mratibu wa Programu ya uongozi na Maadili wa kanisa hilo, Dkt Charles Sokile katika semina na viongozi na wakuu wa taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi za ndani na nje ya Tanzania iliyohusu maadili.
Tuishi na kuhimiza maadili kwa viongozi wetu, ukiona viongozi hawapo katika maadili mema wazomeeni na sio kuwashabikia. Kila mtu awe kiranja kwa mwenzake ukiona mtu haishi katika misinhgi ya maadili paza sauti kwa umma,” amesema Dkt Sokile.
Dk Sokile amesema wanaungana na Rais Samia Suluhu Hassan kwamnba suala la malezi na maadili linaanzia katika familia badala ya kuiachia Serikali peke yake.
“Wazazi wana nafasi nzuri kuishi kwa mfano wa maadili kwa watoto, pili kuwalekeza katika njia sahihi ya maadili. Vita ya maadili na uadilifu tutaishinda kwa kuanzia kwenye ngazi ya familia, tukifanya hivi na viongozi wa dini wakatimiza wajibu wao, tutafanikiwa,” amesema Dkt Sokile.
Mchungaji mwandamizi wa kanisa hilo, Dkt Lucas Shallua amesema kila mtu ni kiongozi, akisema uongozi una maeneo kadhaa ikiwemo uongozi binafsi, wa familia na katika eneo la kazi.
Amesema maeneo hayo yakitiliwa mkazo yatasaidia kubadilisha jamii ya Kitanzania na kuishi katika maadili na uadilifu.