Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amepokea dozi yake ya kwanza ya chanjo ya virusi vya corona ya AstraZeneca.
Merkel mwenye umri wa miaka 66 amedungwa chanjo hiyo kwenye kituo maalumu cha utoaji chanjo kilichojengwa katika uwanja wa zamani wa ndege wa Tampelhof ambao kwa sasa unatumiwa makhsusi na AstraZeneca chanjo ambayo inatolewa tu kwa watu wenye umri wa zaidi ya miaka 60 nchini Ujerumani.
Habari ya kuchanjwa kwa Merkel imetolewa na msemaji wake Steffen Seibert kupitia ujumbe wa mtandao wa kijamii wa Twitter. Merkel ameelezea furaha yake baada ya kupata dozi ya kwanza ya chanjo, na kuwashukuru waote wanaoshiriki kampeni hiyo na wale wanaochanjwa, akisema chanjo ni muhimu katika kulishinda janga la virusi vya corona.