Ikiwa imesalia miezi 4 hadi Uchaguzi Mkuu kufanyika nchini Marekani, rapa Kanye West (43) ametangaza kupitia mtandao wa Twitter kuwa atagombea Urais.
Uchaguzi Mkuu unatarajiwa kufanyika mwezi Novemba. Hata hivyo, zoezi la kuongeza wagombea binafsi bado halijafungwa kwenye majimbo mengi nchini humo.
Baada ya Kanye kuweka ujumbe kuwa atagombea Urais, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tesla, Elon Musk alimjibu akisema anamuunga mkono.