Karibia watu 225 wakiwemo watoto, wameripotiwa kufariki kwa njaa katika eneo linalokabiliwa na ukame na mapigano la Tigray nchini Ethiopia tangu mwezi Julai mwaka jana kwa mujibu wa maofisa katika eneo hilo
Vifo 209 vimeripotiwa katika eneo la Edga Arbi kama walivyothibitisha maofisa kwenye eneo hilo waliozungumza na televisheni ya eneo hilo.
Katika maeneo mengine, watu 16 waliotoroka makazi yao kutokana na vita vya ndani vya miaka mwili vilivyokamilika mwaka wa 2022 wamefariki kutokana na makali njaa.
Maofisa katika jimbo la Tigray awali walikuwa wameonya kuwa baa la njaa ambalo lilitokea nchini Ethiopia katika miaka ya 80 ambapo mamia kwa maelfu ya watu wakiwemo watoto walifariki huenda ikatokea tena.
Licha ya onyo hilo kutoka kwa maofisa wa Tigray, serikali ya shirikisho imekanusha kuwepo kwa baa kubwa la njaa ikieleza kuwa inafanya kazi kutoa chakula cha msaada.