Karim Benzema ameachwa nje ya kikosi cha Al Ittihad kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa wa AFC dhidi ya Navbahor ya Uzbekistani siku ya Alhamisi huku kukiwa na uhusiano mgumu na kocha wake Marcelo Gallardo, chanzo kilithibitishwa na ESPN.
Gallardo haoni kwamba Benzema anafaa vya kutosha kwa safari hiyo baada ya mshindi huyo wa Ballon d’Or 2022 kurejea akiwa amechelewa kwenye kambi ya timu yake ya Dubai wakati wa mapumziko ya majira ya baridi kali Saudia alipokuwa amekwama Mauritius kwa sababu ya dhoruba japo mchezaji mwenyewe anahisi yuko sawa na yuko tayari kucheza, kulingana na chanzo.
Mchezo wa Al Ittihad na Navbahor ni mkondo wa kwanza wa hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa ya AFC.
Benzema hakushiriki katika mechi ya timu yake kurejea Saudi Pro League wiki iliyopita dhidi ya Al Tai, ambayo Al Ittihad ilishinda 3-0 na kutokuwepo huko kulikuja baada ya mzozo kati ya Benzema na Gallardo kuhusu ushiriki wa mchezaji huyo kwenye mazoezi.