Golikipa wa zamani wa klabu za Simba na Dar Es Salaam Young Africans, Juma Kaseja baada ya kukaa nje ya uwanja kwa Zaidi ya miezi sita vipi kastaafu soka kimyakimya au bado tutegemee kumuona akirudi uwanjani?
Kwa muda aliokaa nje ya uwanja golikipa huyo ni muda mrefu kiasi cha watu kujiuliza maswali mengi ikiwemo kuhisi kwamba kastaafu kucheza Soka !!
Kaseja bado hana timu ila aliwahi kuvichezea vilabu pacha kwa awamu mbili tofauti kabla ya kuhitilafiana kimkataba na iliyokuwa klabu yake Yanga hadi kufikia hatua ya Kaseja kufunguliwa kesi Mahakamani, team ya millardayo.com iliongea na Kaseja juu ya kimya chake kingi katika soka.
“Unajua mimi bado nacheza mpira na nitacheza sana… kila mtu amekuwa akiongea la kwake Juma mzee, mimi nilianza kucheza mpira bado mdogo na nimesikika masikioni mwa watu kwa muda mrefu kwa sababu nilikuwa nipo kwenye kiwango kwa muda mrefu, mimi nitarudi uwanjani na nitacheza kwa kiwango cha juu“>>>Kaseja
Sehemu ya Exclusive ya Interview na Kaseja iko kwenye hii sauti hapa.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos