Mradi wa mabasi yaendayo kasi upo chini ya kampuni ya Starbag ambayo zaidi ya kuajiri wafanyakazi wa kigeni pia imeajiri wafanyakazi wa hapa hapa Tanzania.
Wafanyakazi kutoka Tanzania wametoa malalamiko yao na kusema kwamba wanabaguliwa kwenye ulipwaji wa posho zao.
Mmoja wa wafanyakazi hao amesema kwamba wanadai posho kwa miezi zaidi ya mitano na kila mfanyakazi anadai zaidi ya laki tano. Mwingine amesema kwamba wafanyakazi wakigeni wanalipwa posho zao kwa wakati kasoro wafanyakazi kutoka Tanzania kitu ambacho kimewafanya wagome kuendelea na kazi.
Jumla ya wafanyakazi waliogoma ni zaidi ya 1000 na wameenda kwenye makao makuu ya ofisi za Starbag lakini mabosi wa kampuni hiyo hawakutoa ushirikiano kwa mwanahabari aliyekuwa anafuatilia habari hii.
Video credit : ITV