Mbunge wa jimbo la ulanga, Salim Hasham ametembelea katika kata ya mwaya kujionea uharibifu uliojitokeza wa baada ya Sarah’s kuvunjika linalounganisha kata za mwaya, Ilonga, Mbuga na Ketaketa.
Mbunge huyo amesema kwasasa amesharipoti changamoto hiyo kwa mamlaka husika na hatua za haraka zitachukuliwa pia amewapongeza wananchi kwa kujitolea michango ya fedha kiasi cha 1,200,000/= kwaajili ya ujenzi wa kivuko cha muda na yeye amewasapoti kwa kuchangia 1,000,000/= pamoja na mwenyekiti wa halmashauri kutoa 300,000/=, ambapo kwa jumla ilipatikana kiasi cha 2,500,000/=.
Amewataka wananchi kushirikiana na wataalamu katika ujenzi wa kivuko hicho cha muda kipindi ambacho anaendelea kupambana kupata madaraja imara ili kurejesha huduma za kijamii kama hapo awali.