Katibu Mkuu Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres ametoa wito kuwa kusiwepo na upendeleo katika ugawaji wa chanjo ya virusi vya corona na kwamba kila nchi ina haki ya kupata chanjo hiyo zikiwemo nchi za Afrika.
Akizungumza kwa njia ya video kwenye mkutano na Umoja wa Afrika, Guterres amesema anaona utaifa ukipewa kipaumbele kwenye suala la chanjo huku nchi tajiri zikipewa nafasi kubwa kuliko maskini.
“Bidhaa ya umma inapatikana kwa watu wote, kila mahali duniani na hasa barani Afrika ambako kuna mahitaji makubwa ya kukabiliana ipasavyo na msukosuko huo” Guteres
Hivi karibuni shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International, lilifichua kuwa nchi tajiri duniani zimenunua chanjo mara tatu zaidi ya zinavyohitajika, jambo ambalo linaweza kuwakosesha chanjo mabilioni ya watu katika nchi masikini.