Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo amewataka Watanzania wasikubali kupotoshwa kuhusu Mkataba wa Bandari ambapo amesema mkataba huo ni wa CCM na sio Mtu mmoja huku akisisitiza kuwa suala hilo lipo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2020 Ibara ya 59 ukurasa wa 92 kuhusu uboreshaji wa Bandari.
Chongolo amesema hayo wakati akihutibia Wananchi wa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Ruanda Nzovwe, Jijini Mbeya ambapo amesema kuna Watu wametengeneza uongo ili kupotosha uboreshaji wa Bandari nchini “Serikali imepewa msukumo na Chama kinasimamia kuhakikisha utekelezaji unafanyika, naagiza Serikali ichakate haraka kuelekea kwenye mkataba wa uwekezaji wa Bandari”
“Kazi ya maneno ya siasa ni ya Wanasiasa, Watendaji wasihangaike kujibu, eti jambo la fulani hata angekuwa nani ndani ya CCM ajenda isiyo na maslahi ya Watu haitapita”
Chongolo amesema takwimu zinaonesha kuwa Bandaei kwa sasa inaingiza zaidi ya Tsh trilioni 7 huku asilimia 99 ya fedha hizo ikitumika kwa matumizi yao wenyewe “Nani anakula hizo trilionii 7? sasa wakiambiwa ulaji unakatwa watafunga midomo? kuna genge la Watu wanamlo na hawataki kuona