Rais Mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha DSM (UDSM) amefika hosteli za chuo hicho ‘Hostel za Magufuli’ kwa ajili ya kukagua mazingira ya Hostel kabla ya kuanza kuwapokea wanafunzi ambao wanatarajiwa kuendelea na masomo yao June 01, 2020.
Mstaafu Kikwete amesema Serikali imemuhakikishia kuwa Hosteli hizo ambazo zilibadilishwa matumizi na kuwa Karantini kwa Watu wanaotoka nje ya Nchi ikiwa ni hatua ya kupambana na corona, zipo salama tayari kwa matumizi.
“Serikali ilipoamua kuwa kila anayetoka nje ataletwa hapa, shaka yangu ilikuwa itakuwaje kama hawa Watu watakuwa na maradhi, wakiondoka hawatoacha mbegu na Vijana wetu wakija wakaja kupatia maradhi hapa lakini walinihakikishia kwamba Serikali itahakikisha panakuwa salama, nilipata matumaini na nikawaambia lazima tuhakikishe kweli linafanyika” –MSTAAFU KIKWETE
MAAGIZO YA RC MWANRI KWA MA-DC “MSIPOTOA MAELEKEZO MTAPATA MATATIZO”