Mgombe wa Urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, ameweka wazi kuwa kauli mbiu itakoyobeba ilani yao ya chama ni ‘Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watanzania’.
Kauli hiyo ya Lissu ameitoa akiwa Jimbo la Kawe ambapo amesema, chochote kilichopo kwenye ilani kinabeba msingi wa kauli mbiu hizo..
“Ilani yetu ya Uchaguzi Mkuu huu ina kauli mbiu yenye maneno yafuatayo, ‘Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watu’, chochote ambacho tumekisema katika ilani hii msingi wake ni uhuru wa watu msingi wa watu na maendeleo ya watu” Lissu
“Maendeleo tunayoyataka ni yanayozingatia uhuru wa watu, yanayozingatia haki zao, maendeleo aliyoyaita Baba wa Taifa maendeleo ya watu badala ya vitu” Lissu