Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai amemuapisha Prof. Shukrani Manya kuwa mbunge rasmi huku akitoa wito kwa wabunge wa ACT Wazalendo kutoa taarifa ili wapangiwe kuja kuapishwa na kuwatumika wananchi.
Akizungumza mara baada ya kiapo cha Prof. Manya jijini Dodoma, Ndugai amempongeza mbunge huyo kwa kuteuliwa kuwa mbunge huku akisema bunge hilo haitaki kurudisha nyuma kasi ya serikali.
“Nitoe wito kwa wabunge wengine wowote wale, kumbukumbu zangu zinaonesha kuna wabunge wanne wa ACT Wazalendo ambao bado hawajaapa ningetoa wito kama wenyewe wakiwa tayari kutumikia nchi yao kama kweli waliomba ubunge kutumikia wananchi hawana sababu ya kuzurura huko walipo watoe taarifa kwa spika haraka tuwapangie ili wapate kiapo waweze kufanya kazi ya mbunge” Ndugai