Kuna taarifa ambazo kama ukibahatika zikakufikia, zinaweza kukuacha kinywa wazi ama kukushtua kwa namna fulani.
Stori ambayo nimeipata hivi punde kutoka 254 Kenya inahusiana na mazishi ya aina yake ambapo familia moja imefanya mazishi ya mzee wao aliyekuwa akifahamika kwa jina la Adriano Aluchio anayetajwa kuwa mzee wa kuheshimika kwenye jamii hiyo akiwa amekaa ndani ya jeneza lilichongwa kwa namna ya kipekee tofauti na ilivyozoeleka.
Baadhi ya watu waliohojiwa kuhusiana na tukio hilo wamesema ni utamaduni wa jamii ya kabila la Lughia kufanya mazishi ya namna hiyo kwa mzee aliyeheshimika, kwa imani kuwa amefariki lakini anaendelea kuwalinda watoto wake pamoja na jamii yake.
Moja ya wazee katika jamii hiyo amenukuliwa akisema, “Mazishi kama hayo ya kumkalisha marehemu yalianza tangu zamani sana wakati wa mfalme Nabongo Mumia, na sisi tulitokea katika jamii hiyo, tukimzika amelala hatoridhika… Ataonekana akitembea huku juu….”
Baada ya mazishi hayo ya kipekee, walichukuliwa ng’ombe dume wawili na kupiganishwa juu ya kaburi kama njia ya kufukuza mapepo wachafu, huku wanakijiji wakipongeza kitendo cha mzee huyo kupewa mazishi ya hadhi.
Jamii ya Waidakho katika kabila la Walughia wanoishi katika kaonti ya kakamega wanajulikana sana kwa mchezo wao unaowavutia watalii eneo hilo la kuwapiganisha Fahali na kuku Jogoo.