Umoja wa Ulaya na nchi ya Kenya zimetiliana saini makubaliano kuhusu mkataba wa kibiashara baiana yao, hatua inayokuja wakati huu EU ikitafuta uhusiano wa kina wa kiuchumi na Afrika.
Mara baada ya kuidhinishwa na kuanza kutumika, mpango huo wa kibiashara unatarajiwa kuipa Kenya kufikia soko la Ulaya ambapo inatuma sehemu kubwa ya mauzo yake nje.
Kenya inatuma bidhaa zake za kilimo kama vile chai na kahawa maarufu nchini humo na asilimia 70 ya maua yake kwa nchi za kigeni.
Waziri wa Biashara Moses Kuria aliitaja hatua hiyo kuwa “wakati wa fahari” kwa nchi, baada ya kutia saini Mkataba wa Ushirikiano wa Kiuchumi wa EU-Kenya (EPA) na Kamishna wa Biashara wa EU Valdis Dombrovskis.
EU ni mojawapo ya soko kubwa la Kenya na inauza takribani moja ya tano ya mauzo yake yote huko – inasheheni bidhaa nyingi za kilimo ikiwa ni pamoja na mboga mboga, maua , chai na kahawa.
Kenya pia inatarajiwa kupunguza vikwazo kwa bidhaa za Umoja wa Ulaya hatua kwa hatua.
Mkataba huu iliyotia saini Kenya, unafuatia majadiliano ya muda mrefu, ambapo tangu mwaka 2016 nchi wanachama za jumuiya ya Afrika Mashariki zilikataa kutia saini ushirikiano huu kwa kile zilisema utanufaisha zaidi Ulaya kuliko Afrika.