Miili 7 mpya imepatikana huku uchimbaji ukiendelea katika msitu wa Shakahola nchini Kenya siku ya Jumatatu
Huku uchimbaji ukiendelea Jumatatu katika msitu wa Kenya ambapo mamia ya waathiriwa wa ibada ya siku ya maangamizi walipatikana wakiwa wamezikwa mwaka jana, miili saba zaidi iligunduliwa.
Jumla ya watu waliofukuliwa kutoka kwa makaburi ya halaiki sasa inafikia 436.
Serikali ilisitisha uchimbaji wa miili hiyo mwaka jana, ili kuruhusu ulinganifu wa DNA za miili hiyo. Kufikia sasa, ni 34 tu kati ya waathiriwa ndio wametambuliwa.
Miili ya kwanza iligunduliwa Aprili 2023 katika msitu wa Shakahola karibu na pwani ya Kenya, na kusababisha kukamatwa kwa mchungaji Paul Mackenzie ambaye anadaiwa kuwaongoza wafuasi wake kujiua kwa njaa ili “kukutana na Yesu”.
Mackenzie amekana mashtaka 191 ya mauaji, kuua bila kukusudia na ugaidi. Pia ameshtakiwa kwa mateso na ukatili wa watoto.