Azimio la Umoja One Coalition, kiongozi wa chama Raila Odinga amefutilia mbali mkutano wa hadhara wa Kmunkunji uliokuwa ukitarajiwa.
Akihutubia wanahabari Jumatano alasiri, Odinga alisema hatua hiyo ilichochewa na hatari kubwa ya ukosefu wa usalama inayotokana na machafuko yanayoshuhudiwa katika baadhi ya maeneo ya taifa, akiongeza kuwa hatataka kuzidisha hali hiyo.
Raila alidai ripoti za kijasusi zilionyesha kuwa wahalifu waliojihami walikuwa wakijaribu kuwashambulia viongozi wa Azimio.
“Tumejaribiwa kwa moto mara nyingi lakini ni jukumu letu kujikomboa, haikuwa rahisi lakini lazima ifanyike,” Raila alisema.
Kwa sasa watu watatu wamethibitishwa kufariki eneo la Mlolongo baada ya mabishano kati ya waandamanaji na polisi.
Mwanamume mmoja ameuawa kwa kupigwa risasi wakati wa maandamano katika mji wa Emali nchini Kenya, takriban kilomita 100 kutoka mji mkuu wa Nairobi, kulingana na ripoti nyingi katika vyombo vya habari vya ndani.
Maafisa wa Kenya waliwarushia vitoa machozi waandamanaji walipokaidi marufuku ya polisi kujiunga na maandamano yaliyoitishwa na kiongozi wa upinzani Raila Odinga kupinga msururu wa nyongeza ya ushuru.