Muswada dhidi ya wapenzi wa jinsia moja unaopendekezwa nchini Kenya unataka watu wa mapenzi ya jinsia moja kufungwa jela hadi miaka 50 .
Ukiitwa Muswada wa Ulinzi wa Familia wa 2023, rasimu ya sheria inayofadhiliwa na mbunge wa Homa Bay Town Peter Kaluma, inapendekeza kupiga marufuku mapenzi ya jinsia moja, miungano ya watu wa jinsia moja na shughuli na kampeni zozote za LGBTQ.
Pia inalenga kupiga marufuku maandamano ya watu wa mapenzi ya jinsia moja, mikusanyiko na maandamano barabarani, na mavazi ya yanayoashiria kuwa mpenzi wa jinsia moja hadharani.
“Mtu anayeshiriki tendo la ndoa na mtu wa jinsia moja bila ridhaa ya mtu mwingine atapatikana na hatia atahukumiwa kifungo kisichopungua miaka 10 na kisichozidi miaka 50,” unasema muswada huo.
Wamiliki wa majengo yanayotumika kwa mapenzi ya jinsia moja watalipa faini ya $14,000 (£11,000) au watakabiliwa na kifungo cha miaka saba jela iwapo muswada huo utakamilika.
Kulingana na BBC wiki iliyopita, makasisi na baadhi ya mashirika ya kijamii yalifanya maandamano ya kupinga LGBTQ katika mji wa pwani wa Mombasa.
Hii ilifuatia kutekelezwa tena na Mahakama ya Juu ya Kenya kwa uamuzi wa katikati ya Septemba kuruhusu usajili wa mashirika yasiyo ya kiserikali ya LGBTQ.
Bodi ya Kuratibu Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya Kenya ilikataa kusajili Tume ya Kitaifa ya Haki za watu wa mapenzi ya jinsi moja, ikisema “inakuza tabia ya watu wa jinsia moja”.