Wizara ya afya ya Kenya inasema mwanamume ambaye ni dereva wa lori mwenye historia ya kusafiri kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (D.R.C.)amepatikana na virusi vya ugonjwa wa Homa ya Nyani au Mpox.
Derva huyo alijitokeza kuchunguzwa katika mji wa Busia magharibi mwa Kenya.uliopo katika mpaka wa nchi jirani ya Uganda.
Sampuli yake ya maabara ilithibitishwa kuwa na virusi na tangu wakati huo ametengwa na yuko chini ya uangalizi thabiti.
Aidha uchunguzi wa kina kwa watu wanaoshukiwa kuwa na virusi vya Mpox umeimarishwa katika eneo hilo na katika kaunti zote ili kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo.
Tukio la kwanza pia lilikuwa dereva wa lori la masafa marefu. Alikuwa akisafiri kutoka Uganda kuelekea Rwanda kupitia Kenya, Wizara ya Afya ilisema wakati huo.