Ikiwa timu ya Taifa ya Tanzania ipo Algeria tayari kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa kuwania kufuzu kucheza Kombe la Dunia mwaka 2018 Urusi dhidi ya timu ya taifa ya Algeria katika mji wa Blida uwanja wa Mustapha Tchaker Jumanne ya November 17, majirani zao wa Kenya bado wanaripotiwa kukwama uwanja wa ndege kwa muda sasa.
Timu hiyo ya taifa ya Kenya Harambee Stars imeshindwa kusafiri kuelekea Cape Verde na kukwama katika uwanaj wa ndege wa Wilson baada ya kampuni ya ndege iliyokuwa inatajwa kuingia makubaliano ya kuisafirisha kugoma kuruhusu ndege hiyo iondoke hadi wakamilishiwe malipo yao yote kwani hawana imani na shirikisho la soka la Kenya KFF kama litalipa deni.
Harambee Stars ambao wanapaswa kwenda Cape Verde kucheza mchezo wa marudiano wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2018 Urusi dhidi ya Cape Verde baada ya mchezo wa awali uliochezwa Kenya na Harambee Stars kuibuka na ushindi wa goli 1-0, wanakabiliwa na ukata kwa muda sasa hata awali waliripotiwa wachezaji kudai malimbikizo ya posho zao.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE.