Usiku wa November 16 wachezaji wa kikosi cha timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars walikwama uwanja wa ndege wa Wilson Kenya baada ya wamiliki wa ndege Skyward Express Limited kugoma kuruhusu ndege ipae hadi walipwe malipo yao yote ya umbali wa kilomita 6955 za kwenda Cape Verde kabla ya usiku wake kuripotiwa mipango kukamilika na wachezaji kusafiri.
Safari ya timu ya taifa ya Kenya kuelekea Cape Verde ilianza kuwa na mgomo toka hotelini baada ya wachezaji kugoma kwenda uwanja wa ndege hadi walipwe fedha zao zote za malimbikizo ya posho, stori zilikuwa nyingi kuhusu kukwama huko hadi nahodha wa timu hiyo Victor Wanyama anayekipiga katika klabu ya Southampton ya Uingereza kuwasiliana na klabu yake na kumwambia kama safari hiyo anaona kwake sio salama hasiende.
Stori kutoka mediamaxnetwork.co.ke zinaripoti kuwa Rais wa shirikisho la soka la Kenya (FKF) Sam Nyamweya anatajwa kushitakiwa kwa kosa hilo na baada ya kusababisha wachezaji kukaa uwanja wa ndege wa Wilson kwa masaa 10, Kenya ambao watacheza na Cape Verde katika mchezo wa pili wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2018, kama wasingeenda Cape Verde basi wapinzani wao Cape Verde wangepewa ushindi wa mezani wa goli 3-0 na Kenya kupigwa faini ya dola milioni moja na FIFA kwa mujibu wa sheria za FIFA (articles 31 and 56 of the Fifa Disciplinary Code)
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.