Kulingana na shirika la Africa Network for Animal Welfare ,kati ya mwaka wa 2018 na 2021 idadi ya punda nchini Kenya ilipungua kutoka millioni 1.8 hadi millioni 1.1.hali ambayo ilisabisha serikali kufunga machinjio ya punda.
Hatua hiyo ya serikali ya Kenya imesaidia idadi ya Punda kuongezeka na kurudisha matumaini kwa wafugaji wanaotegemea mnyama huyo muhimu kwaajili ya shughuli za kila siku.
Ngozi ya Punda ina hitaji kubwa katika masoko ya uchina kwa utengenezaji wa dawa iliyopewa jina la Ejiao,ambayo inaaminika kupunguza uzee kwenye mwili wa binadamu.
Hata hivyo wafugaji wameonywa dhidi ya kuwalisha Punda bangi ili wafanye kazi kwa muda mrefu bila kuchoka.
Uwepo wa machinjio vya punda nchini Kenya ulisababisha idadi ya punda kupungua huku wizi ukizidi hasa maeneo kame ambapo punda hao hutumika kwa wingi.
Kundi hilo la mtandao wa watetezi wa haki za wanyama, (ANAW) lilimesema kuwa punda wamekuwa wakitoweka haraka sana na
ripoti ya mwaka 2020 ilisema tangu kufunguliwa kwa maeneo manne ya machinjio ya punda kwa ajili ya biashara mwaka 2016, idadi kubwa ya wanyama hao walichinjwa kila siku”.