Wakenya wamepewa Mapumziko maalum ya kitaifa na kupanda miti milioni 100 kama sehemu ya lengo la serikali kupanda miti bilioni 15 katika kipindi cha miaka 10.
Likizo hiyo inaruhusu “kila Mkenya kumiliki mpango huo”, kulingana na Waziri wa Mazingira Soipan Tuya.
Kila Mkenya anahimizwa kupanda angalau miche miwili, hivyo basi kufikia lengo la milioni 100.
Mpango huo unanuiwa kusaidia kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Miti husaidia kukabiliana na ongezeko la joto duniani kwa kunyonya kaboni dioksidi kutoka angani huku ikitoa oksijeni angani.
Serikali inatoa takriban miche milioni 150 katika vitalu vya umma.
Inatoa miche hiyo bila malipo katika vituo vya wakala wake wa misitu ili Wakenya wapande katika maeneo maalum ya umma.
Lakini pia imewahimiza Wakenya kununua angalau miche miwili ili kuipanda katika ardhi yao wenyewe.