Rais wa Kenya Uhuru Kenyata, leo ijumaa April 24 ametangaza kuwa Wakenya waliopo nchini China watatumiwa ndege itakayowarudisha nchini humo mnamo May 1 mwaka huu.
Akitangaza uamuzi huo, Rais Kenyata amesema Serikali ya nchi hiyo itatuma ndege ya shirika la Kenya Airways ikitokea Jijini Nairobi kuelekea katika Jiji la Guanzhou nchini China kwa ajili ya kuwasafirisha Wakenya wote waliokwama katika nchi hiyo na ambao wameomba kurudishwa nchini mwao.
Balozi wa Kenya nchini China, Sarah Serem amesema hatua hiyo inafuatia maombi ya Wakenya wengi waliopo nchini China waliopaza sauti ya kubaguliwa na wenyeji na wakiiomba Serikali ya nchi yao kuwarudisha nyumbani.
“Serikali ya Kenya imetoa ndege itakayowarudisha nyumbani wakenya wote ambapo nauli imepunguzwa mpaka Ksh 80,000 kwa daraja la ‘economy’ kuwawezesha wakenya watakaotaka kurudi nyumbani kumudu gharama za usafiri” Sarah Serem.