Idadi ya visa vya ugonjwa wa Mpox nchini Pakistani imeongezeka hadi watu watano kufuatia uthibitisho wa virusi hivyo kwa abiria wa ndege huko Peshawar huku kisa kinachoshukiwa kuwa na virusi hivyo kikigunduliwa huko Karachi, maafisa wa afya walisema Jumamosi, Agosti 31, 2024.
Irshad Ali, Mkurugenzi wa Afya ya Umma wa mkoa wa kaskazini-magharibi wa Khyber Pakhtunkhwa, alisema wafanyikazi wa matibabu katika uwanja wa ndege waligundua wasafiri wawili wakirudi kutoka Jeddah wakionyesha dalili za mpox siku ya Alhamisi na ni mmoja tu kati yao aliyethibitishwa kuwa na mpox.