Usikilizwaji wa kesi kutoka pande zote za utetezi na mashtaka wa shauri la Polisi wa zamani wa Jiji la Minneapolis, Derek Chauvin, ambaye anashtakiwa kwa mauaji ya Mmarekani mweusi, George Floyd, unaanza leo Machi 29.
Kesi hiyo ambayo itasikilizwa na watu 12 wanaounda baraza la mahakama wanatarajia kusikiliza ushuhuda katika kesi hiyo inayotarajiwa kuchukuwa mwezi mzima kukamilika.
Afisa huyo wa Polisi ambaye ni mzungu amepinga mashtaka yote yanayomkabili yanayohusu mauaji ya mwanaume mweusi, George Floyd.
Awali, alijitetea kwa kusema alichokifanya kiliendana na mafunzo ya kipolisi aliyopewa wakati alipokuwa akimkamata George Floyd.