Leo February 03, 2020 Mahakama ya Katiba Malawi inatarajia kutoa hukumu katika kesi ya kupinga matokeo ya Urais baada ya Tume ya Uchaguzi kumtangaza Peter Mutharika kuwa mshindi wa uchaguzi wa Urais uliofanyika May 21, 2019.
Dr. Lazarus McCarthy Chakwera wa Chama cha Malawi Congress (MCP) na mwenzake wa Chama cha United Transformation Movement (UTM) Dr Saulos Chilima walifungua kesi katika Mahakama ya Katiba August 8 , 2019.
Kesi hiyo ni ya kuomba kufutwa kwa matokeo ya Urais, na leo February 3 , Mahakama ya katiba inatoa hukumu yake.
Video inaonesha Wanajeshi wakiwa wanaingia eneo la Mahakama ili kuimarisha ulinzi.
Via: Ephraim Mkali Banda,
Security and Diplomacy Journalist